loader
Wenye watoto watoro kupandishwa kizimbani

Wenye watoto watoro kupandishwa kizimbani

Ofisa Taaluma wa Mkoa wa Mwanza, Gervas Sezulu alisema hayo jana katika mahojiano na gazeti hili kuhusu hatua zitakazochukuliwa kwa wazazi ambao hadi sasa watoto wao hawajaripoti sekondari bila taarifa.

Alisema hadi kufikia mwishoni mwa Machi mwaka huu, asilimia 27 ya wanafunzi waliochaguliwa kujiunga na sekondari, walikuwa hawajaripoti shuleni licha ya baadhi yao kwenda kwenye shule binafsi.

Akifafanua zaidi Sezulu alisema wanafunzi 24,347 kati ya 33,200, sawa na asilimia 73 ndio walioripoti shuleni hadi sasa huku wanafunzi 8,853 wakiwemo wavulana 4,794 na wasichana 4,059 wakiwa hawajaripoti.

Wilaya ya Magu inaongoza kwa kuwa na idadi kubwa ya wanafunzi ambao hawajaripoti shuleni, inayofikia asilimia 40, ikifuatiwa na Wilaya ya Sengerema asilimia 37.3, Ukerewe asilimia 31.7 na Kwimba asilimia 30.

Wilaya ya Misungwi ina asilimia 28.5 ya wanafunzi ambao hawajaripoti, Nyamagana ni asilimia 17.1 na Ilemela ni asilimia 6.2.

Alisema mwaka 2013 asilimia 22 ya wanafunzi hawakuripoti sekondari kutokana na sababu mbalimbali, ikiwemo wazazi kutokuwa tayari kuwapeleka, tabia ya mtoto mwenyewe, na utoro wa baadhi waliokimbilia kwenye ufugaji na uvuvi pamoja na kuolewa.

Kutokana na idadi kubwa ya wanafunzi kutoripoti shule, Sezulu aliwataka viongozi watoe msisitizo kwa wazazi kuhusu umuhimu wa kupeleka watoto wao shule na kupata elimu.

Alitaka msukumo huo uanzie ngazi ya Mkoa, Wilaya na kwa Madiwani ambao utasaidia kubadili tabia iliyopo ili watoto wasipotee kwa kukosa elimu.

Ametoa mwito kwa wazazi waliohifadhi watoto wao licha ya muda kupita, wawapeleke shule kwani nafasi zao bado zipo.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia ...

foto
Mwandishi: Grace Chilongola, Mwanza

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi