loader
Dstv Habarileo  Mobile
Wizara: Madini hayaibwi

Wizara: Madini hayaibwi

Imeelezwa kuwa madini hayo hupitia Wakala wa Ukaguzi wa Madini Tanzania (TMAA), hivyo hukaguliwa na kusimamiwa ipasavyo.

Hayo yalibainishwa mjini hapa juzi na Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Eliakim Maswi alipotembelea na kukagua maendeleo ya mgodi wa makaa ya mawe wa Ngaka unaoendeshwa kwa ubia kati ya Kampuni ya Australia ya Tancoal na Shirika la Maendeleo ya Taifa (NDC).

Alisema TMAA wapo katika kila mgodi nchini kwa ajili ya kusimamia na kukagua kiasi cha madini kinachochimbwa na kuuzwa ikiwa ni pamoja na kuhakiki vyeti vya mauzo ya madini hayo kwa kuhakikisha kuwa vinakwenda sambamba na kiasi cha mrabaha kinachotolewa na wawekezaji.

“Serikali imejipanga kuhakikisha kuwa sekta hii ya madini inawanufaisha Watanzania na si kuishia mikononi mwa wachache, ndio maana kuna TMAA ambao kazi yao ni kusimamia na kukagua kila kitu kinachoendelea katika migodi yetu yote hapa nchini,” alisema Maswi.

Kamishna wa Madini nchini, Paul Masanja alisema Serikali kupitia maofisa hao wa TMAA wamekuwa wakifanya ukaguzi kuhakikisha kwamba Serikali inapata mrabaha stahili kupitia madini yanayouzwa ambapo alibainisha kuwa katika madini ya makaa ya mawe ya Ngaka Serikali inapata asilimia 100 ya mrabaha.

Kwa upande wake, Mkurugenzi wa Tancoal, Tan Brereton alisema mgodi huo ni mradi mkubwa kwa Tanzania, kutokana na ukweli kuwa makaa yanayozalishwa hapo ni ya kiwango cha hali ya juu tofauti na migodi mingine kutoka nchi za jirani ikiwemo Afrika Kusini.

Aidha alisema kutokana na uwepo wa kiasi kikubwa cha makaa hayo ya mawe katika mgodi huo unaokadiriwa kuwa na akiba ya tani milioni 450 itakayodumu na kutumiwa kwa takribani miaka 200, itawezesha kuuzwa kwa makaa hayo ndani na nje ya nchi, lakini pia kutumika katika kuzalisha umeme.

“Makaa haya ya Ngaka yana ubora wa hali ya juu sana tofauti na makaa yanayochimbwa Afrika Kusini kwa kuwa madini haya hayahitaji kusafishwa baada ya kuchimbwa kabla ya matumizi tofauti na mengine ambayo husafishwa kabla ya kutumiwa, alisema Brereton.

Sehemu kubwa ya ulimwengu wa biashara uli dorora kutokana na ...

foto
Mwandishi: Halima Mlacha, Mbinga

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi