loader
Yamaha yawezesha waendesha pikipiki

Yamaha yawezesha waendesha pikipiki

Aidha kampuni hiyo iliyopo chini ya Kampuni ya Toyota Tanzania Limited imeamua kupunguza bei ya pikipiki zake aina ya Yamaha kwa lengo la kuwavutia vijana wengi na kuunga mkono jitihada za serikali za kuongeza ajira kwa vijana kupitia biashara ya bodaboda ambayo imesaidia vijana wengi kujiajiri na kuepuka kujitumbukiza kwenye matukio ya uhalifu.

Meneja wa kampuni hiyo tawi la Arusha, Meetal Shah alisema kampuni yake imefikia hatua hiyo ikiwa ni sehemu ya kuchangia ajira kwa vijana kupitia biashara ya bodaboda.

“Tunachokifanya ni kuwaunganisha wateja wa pikipiki wasio na fedha taslimu na benki ambazo zimekubali kuwakopesha kwa riba nafuu na sisi kama Kampuni ya City Motors tutawapatia pikipiki na benki ndiyo itakayotulipa sisi, ’’alisema Shah.

Kwa upande wa waendesha pikipiki, John Jumanne (39) mkazi wa Sombetini aliyepatiwa pikipiki aina ya Yamaha kupitia mpango huo, ameishukuru kampuni hiyo ya City Motors kwa kueleza kuwa kabla ya hapo alikuwa akiendesha pikipiki ya mtu kwa makubaliano ya kumlipa Sh 7,000 kwa siku na hivyo kujikuta akibakiwa na fedha kidogo ambazo hazitoshelezi kutunza familia yake.

WADAU wa Sekta ya Kilimo nchini wameshauriwa ...

foto
Mwandishi: Veronica Mheta, Arusha

Post your comments

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi