loader
Yanga, Chipukizi kucheza Pemba leo

Yanga, Chipukizi kucheza Pemba leo

Akizungumza na gazeti hili jana akiwa Pemba, Meneja wa timu hiyo, Hafidhi Saleh alisema kikosi chao kipo vizuri kwa ajili ya mchezo huo.

Saleh alisema pamoja na mechi hiyo, wako vizuri, na kocha wao mkuu, Marcio Maximo amefurahishwa na kambi hiyo kutokana na utulivu uliopo ambao unamwezesha kufanya kazi yake bila usumbufu.

“Kikosi chetu kipo katika hali nzuri wachezaji wetu wote ni wazima hakuna aliyekuwa majeruhi,” alisema Saleh na kuongeza: “Kocha ameahidi kupanga kikosi kamili ambacho atakuwa akikitumia kwenye mechi za Ligi Kuu ili aweze kujua mapungufu kabla ya ligi kuanza.”

Alisema kambi ya Pemba imeongeza umoja na mshikamano baina ya wachezaji wapya na wale wageni waliokuwa kwenye timu za taifa, jambo ambalo linaleta matumaini ya kufanya vizuri kwenye mechi za Ligi Kuu.

“Huenda lengo la Maximo la kutaka umoja na upendo kwa wachezaji na viongozi likafanikiwa kupitia kambi hii kwa sababu wachezaji wamekuwa na ushirikiano na nidhamu ya hali ya juu wanapokuwa ndani na nje ya uwanja, kitu ambacho kocha alikuwa anakisisitiza,” aliongeza.

Baada ya leo dhidi ya Chipukizi, timu hiyo itacheza michezo miwili ili kukamilisha idadi ya mechi tatu ambazo kocha Maximo, amezihitaji na baada ya hapo timu itarudi Dar es Salaam.

Itarudi kuendelea na maandalizi yake ya mwisho na kucheza mechi mbili kabla ya kuvaana na Azam FC katika mchezo wa Ngao ya Jamii Septemba 13, mwaka huu.

Yanga iliondoka Dar es Salaam na kikosi cha wachezaji 27 ambao Maximo amepanga kuwatumia msimu mpya, lakini inakosa huduma ya mshambuliaji nyota wa kimataifa wa Uganda Emmanuel Okwi ambaye hajajiunga na wenzake.

SIMBA Queens imekuwa timu ya ...

foto
Mwandishi: Mohamed Akida

Post your comments

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi