loader
Dstv Habarileo  Mobile
Yanga yatangaza kushiriki Kagame

Yanga yatangaza kushiriki Kagame

Akijibu maswali ya waandishi wa habari jana Dar es Salaam, Katibu Mkuu, Beno Njovu alisema barua wameipata Ijumaa mchana kupitia Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) ikiwataka wathibitishe ushiriki wao.

Awali, klabu hiyo ilikuwa ikisita kuzungumzia maandalizi kwa madai kuwa walikuwa wakisubiri barua hiyo.

Njovu alisema mpango wao wa kushiriki upo, lakini hawana mpango wa kuipeleka timu kambini kwa vile nusu ya wachezaji wake tegemeo wapo kwenye kikosi cha timu ya Taifa ‘Taifa Stars’ na watarajiwa kuwa huru kuanzia Agosti 5, mwaka huu.

“Hatuwezi kwenda kambini, isipokuwa Kocha Mkuu Marcio Maximo anaendelea na mazoezi, na nusu ya wachezaji wetu wengine ndio hao wapo kwenye kikosi cha Stars,” alisema na kuongeza kuwa sio kweli kwamba wamepanga kupeleka wachezaji wa timu B kama walivyonukuliwa.

Katika michuano hiyo, Yanga ambao wako katika Kundi A, wamepangwa kuanza na Rayon ya Rwanda katika michuano itakayoanza kutimua vumbi Agosti 8, mwaka huu nchini Rwanda.

Kwa mujibu wa ratiba iliyotolewa jana na Meneja Habari wa Baraza la Vyama vya Mpira wa Miguu Afrika Mashariki na Kati (CECAFA), Rogers Mulindwa, Yanga na Rayon Sports watacheza mechi hiyo kwenye Uwanja wa Amahoro mjini Kigali ikiwa ni mechi ya Kundi A.

Kabla ya mechi hiyo, wawakilishi wa Tanzania Zanzibar, KMKM itacheza na Atlabara kwenye Uwanja wa Nyamirambo katika mechi nyingine ya Kundi A ya michuano hiyo ya kila mwaka. Aidha, kutakuwa na mechi nyingine siku hiyo kati ya Gor Mahia na KCCA.

YANGA leo saa 1:00 usiku itashuka dimbani kuikabili ...

foto
Mwandishi: Mwandishi Wetu

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi