loader
ZSTC yanunua karafuu ya bilioni 76/-

ZSTC yanunua karafuu ya bilioni 76/-

Mkurugenzi mtendaji wa Shirika la Taifa la Biashara (ZSTC), Mwanahija Almasi alisema hayo wakati akitoa taarifa mbele ya Rais wa Zanzibar, Dk Ali Mohamed Shein katika uzinduzi wa msimu wa mavuno ya karafuu kwa mwaka 2014-2015 kisiwani Pemba.

Alisema wakulima wengi wa kisiwa cha Pemba wameitikia mwito wa kuuza karafuu zao kupitia ZSTC baada ya kuwepo bei nzuri ya kuvutia ambayo imesaidia kupungua kwa magendo ya karafuu Pemba.

Alisema bei nzuri inayotoa faida kwa mkulima asilimia 80 pamoja na mazingira mazuri ya kununua karafuu ndiyo yaliyowavutia wakulima wengi kuuza karafuu zao kupitia ZSTC na kuachana na magendo yaliyoshamiri katika kipindi kirefu.

Alisema shirika hilo limekamilisha kazi ya kujenga vituo sita vya kununua karafuu vilivyopo Pemba ambavyo vitawafanya wakulima kuuza karafuu katika mazingira salama.

Alisema ujenzi wa vituo hivyo unatokana na agizo la Rais wa Zanzibar, Dk Ali Mohamed Shein la kulitaka shirika hilo kujenga vituo vyenye hadhi ambapo huduma zote muhimu zitakuwa zikipatikana ikiwemo ulinzi.

Awali Waziri wa Biashara, Viwanda na Masoko, Nassor Ahmed Mazrui alisisitiza kwamba Serikali haitolibinafsisha zao la karafuu kuingia katika mikono ya sekta binafsi.

foto
Mwandishi: Khatib Suleiman

Post your comments

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi