Mazao ya biashara kuuzwa kupitia ushirika

WAZIRI Mkuu, Kassim Majaliwa amesema katika msimu huu wa kilimo, mazao yote ya biashara yatauzwa kupitia vyama vya ushirika vilivyopo. Alitoa kauli hiyo jana mjini hapa katika hafla ya uwekaji wa jiwe la msingi katika Mradi wa Ujenzi wa Vihenge na Maghala ya Kisasa ya Wakala wa Taifa wa Hifadhi ya Chakula (NFRA), ambao utafanyika katika kanda nane za wakala.

Add a comment