Benki ya Walimu yarahisisha uchukuaji fedha kwenye ATM

BENKI ya Walimu (MCB) iko mbioni kuanzisha huduma za mashine za kutolea fedha (ATM) bila ya kadi, huduma ambayo itarahisisha wateja wake kupata fedha kutoka kenye mashine hizo bila kubeba kadi yoyote.

Hayo yalisemwa na Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya benki hiyo mjini Morogoro jana, Herman Kessy kwenye mkutano mkuu wa kwanza wa wanahisa wa benki hiyo.

Aidha, aliwaambia wajumbe wa mkutano huo kuwa, benki hiyo pia itaanzisha uwakala wa benki ambayo itashirikiana na mawakala wa sehemu mbalimbali na ili kuhakikisha inafikisha huduma za kibenki kwa wananchi wote kwa urahisi, uhakika na unafuu.

“Kupitia huduma hii, wateja wataweza kupata pesa zao kupitia mawakala au kupakua programu maalumu kwenye simu zao za kiganjani zitakazowezesha kulipa huduma za maji, umeme pia kutuma pesa kutoka kwenye akaunti zao kwenda kwenye huduma maalumu ya benki kwa njia ya simu,” alifafanua.

Akizungumzia hali ya taasisi za kifedha nchini, Kessy alisema MCB iko imara licha ya changamoto zilizojitokeza hivi karibuni kutokana na agizo la serikali kuelekeza taasisi zake zote za umma kuhamisha na kupeleka fedha zote Benki Kuu ya Tanzania (BoT) na hivyo wateja wakubwa wa serikali kufunga akaunti zao na kuhamishia fedha zao BoT.

“Lakini sio hilo tu, hata uhakiki wa watumishi wa umma uliobaini watumishi hewa 19,000 umetuathiri kwa sababu wakati wa uhakiki uliofanyika kwa zaidi ya siku 90 urejeshaji wa makato ulisitishwa, hivyo basi benki ikiwemo yetu hatukupata marejesho ya mikopo kutoka kwa wafanyakazi walioathiriwa na uhakiki huo na pia kukosa mapato yatokanayo na r