Fastjet yanunua Easyjet

KAMPUNI ya Ndege ya Fastjet imenunua hakimiliki zote kutoka kwa kampuni mwenza ya Easyjet kuanzia Juni mwaka huu kwa gharama ya Dola za Marekani milioni 2.5 (Sh bilioni 5.25).

Akitangaza kuhusu uamuzi huo, mwanzilishi na mwanahisa wa Easy- Group, Sir Stelios Haji-Ioannou alisema kampuni yake imechukua uamuzi huo kwa lengo la kujiimarisha zaidi, hasa ikizingatiwa kuwa kwa sasa imetanuka zaidi kibiashara.

Alisema,”Fastjet ni kampuni kubwa kwa sasa inayotoa huduma sehemu nyingi Afrika, kwa hiyo tumeona ni vema tuwauzie haki zote ili wajiendeleze zaidi kibiashara. Aliongeza, kampuni yake ilijadiliana na bodi ya Wakurugenzi ya Fastjet na kukubaliana kuiuzia hisa zake na Fastjet na bila ya kupoteza muda imezinunua.

Pia aliweka wazi kuwa kwa sasa yeye binafsi amebakiza hisa za thamani ya pauni milioni 1.3 zinazomwezesha kuwa mwanahisa na ataendelea kuishauri Fastjet. Ofi sa Mtendaji Mkuu wa Fastjet, Nico Bezuidenhout alisema kampuni yake imenunua hisa hizo kutokea kwa wakati mwafaka kutokea Easyjet.