Mtaka aialika benki ya kilimo

SERIKALI mkoani Simiyu imekutana na viongozi wakuu wa Benki ya Maendeleo ya Kilimo nchini ili kuona jinsi benki hiyo inaweza kuweka nguvu zake katika mkoa huo unaokuwa haraka kwa viwanda.

Akizungumza ofisini kwake jana, Mkuu wa Mkoa huo, Anthon Mtaka aliwataka viongozi hao kuweza kuanza tathimini mara moja ili kujua wanaweza kuwekeza katika kilimo.

Aliongeza kuwa anasononeshwa na vitendo vinavyofanywa na wafanyabiashara wanaokuja Simiyu kununua chakula kwa bei ya chini, mkulima akiuza angalau aweze kupata pesa kwa ajili ya kuendesha familia yake.

Mtaka alisema kwa Kanda ya Ziwa hakuna mkoa wenye uoto wa asili na wenye kuvutia wawekezaji kama mkoa wa simiyu, hivyo sasa hii ni fursa kwa watu kama Benki ya Maendeleo ya Kilimo walivyoiona na kuja kutaka kuwekeza mkoa humu kuweza kuja kujenga viwanda na kutoa ajira kwa watu wake.