Biashara ya alizeti yashamiri Kongwa

BIASHARA ya alizeti imeshamiri katika mji mdogo wa Kibaigwa wilaya ya Kongwa mkoani Dodoma. Wakizungumza hivi karibuni baadhi ya wakulima walisema mwaka huu bei iko juu kutokana na mavuno kuwa machache yalikosababishwa na uhaba wa mvua.

“Mwaka huu gunia moja mpaka sasa tunauza kwa Sh 50,000 hadi Sh 45,000 tofauti na mwaka jana ambapo gunia moja liliuzwa hadi Sh 30,000” alisema mkulima kutoka kijiji cha Ndurugumi, Aidan Rangi. Alisema kutokana na alizeti kuwa chache mwaka huu hata bei ya mafuta inaweza kuwa juu. Alisema wengi wa wakulima wamekuwa wakisafirisha alizeti hiyo