HESHIMA ZA MWISHO

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akitoa heshima za mwisho kwa askari 14 wa Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) waliouawa wakiwa katika operesheni ya ulinzi wa amani chini ya Umoja wa Mataifa nchini Congo (DRC), kwenye viwanja vya Makao Makuu ya JWTZ, Dar es Salaam akimwakilisha Rais John Magufuli, jana.

Add a comment

JENGO LA KITEGA UCHUMI

Rais John Magufuli, Makamu wa Rais, Samia Suluhu Hassan, Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa, Naibu Katibu Mkuu CCM Bara, Philip Mangula na viongozi wengine wakipata maelezo ya ujenzi wa jengo la kitegauchumi la Jumuiya ya Wazazi linalojengwa Ilala Mchikichini, Dar es Salaam na Kampuni ya Elite Consultants kabla ya ufunguzi wa mkutano wa Tisa wa Jumuiya hiyo katika ukumbi wa Jakaya Kikwete Dar es Salaam jana. (Picha na Ikulu).

Add a comment

MKUTANO MAWAZIRI WA SHIRIKA LA BIASHARA DUNIANI

Katibu Mkuu, Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Profesa Elisante Ole Gabriel akiwa katika picha ya pamoja na Maxim Medvedkov (Mkurugenzi Idara ya Majadiliano ya Biashara ya Urusi) na Ekarina E. Mayorova (Mkurugenzi Msaidizi Idara ya Majadiliano ya Biashara ya Urusi) ambao ni sehemu ya ujumbe wa Urusi katika mkutano unaoendelea wa kumi na moja wa Mawaziri wa Shirika la Biashara Duniani (WTO). Moja ya masuala waliyozungumzia ni uwezekano wa kuanzisha majadiliano na kampuni ya Urusi iitwayo Ros Atom kwa ajili ya uwekezaji katika utengenezaji wa kinu cha kuzalisha umeme wa nyuklia Tanzania.

Add a comment

MAZUNGUMZO

Katibu Mkuu Profesa Elisante Ole Gabriel akiwa kwenye mazungumzo na Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Biashara la Dunia (WTO) Roberto Azavedo wakati wa Mkutano wa 11 wa WTO (MC11) mjini Buenos Aires, Argentina.

Add a comment

KUPOKEA MIILI YA ASKARI WALIOUAWA DRC

Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa (JKT), Dk Hussein Ali Mwinyi (kulia) akiongoza askari wa jeshi hilo wakati wa kupokea miili ya askari 14 waliouawa nchini DRC wiki iliyopita. Miili ya askari hao ilipokelewa kwenye Uwanja wa Jeshi (Air Wing) Dar es Salaam jana. (Picha na Iddy Mwema).

Add a comment

KUSAINI NYARAKA ZA MSAMAHA

RAIS John Magufuli akitia saini nyaraka za msamaha alioutoa kwa wafungwa 61 waliohukumiwa kunyongwa hadi kufa. Kushoto ni Kamishna Jenerali wa
Magereza, Juma Malewa akishuhudia tukio hilo lililofanyika katika Ikulu ya Chamwino Mjini Dodoma.

Add a comment