KUKABIDHI HUNDI

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar, Balozi Seif Ali Iddi (wa tatu kushoto) akikabidhi mfano wa hundi yenye thamani ya Dola ya Kimarekani 5,000 kwa mshindi wa kwanza wa mashindano ya Dunia ya kusoma na kuhifadhi Qur’an, Abdulmajid Mujahid Alsamawiy (kulia) raia wa Yemen baada ya kushinda mashindano hayo yaliyofanyika Dar es Salaam. Wa pili kushoto ni Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Kuhifadhi Qur’an Duniani, Dk Abdallah Basfar na viongozi wengine.