AKIPOKEA FUNGUO

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akipokea funguo ya magari matatu yenye thamani ya dola za Marekani 99,700, ambayo amekabidhiwa na Naibu Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Foton International kutoka China, Zhao Xiano kwa ajili ya kusaidia shughuli za maendeleo nchini. Wanaoshuhudia kutoka kushoto ni Meneja Masoko wa kampuni ya Simba Motors Tanzania, Ifigenia Salazar na kulia ni Ofisa Masoko wa Foton International, Fan Liang. Makabidhiano hayo yalifanyika ofisini kwa Waziri Mkuu, Dar es salaam jana.