KARIBUNI NYUMBANI

Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro, Anna Mghwira (kushoto) akiwaongoza wananchi waliofi ka kwenye mapokezi ya wanafunzi wa shule ya Lucky Vicent waliopata ajali, wakirejea kutoka Marekani katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Kilimanjaro jana. Wanafunzi hao ni Doreen Mshana aliyekaa kwenye kiti cha magurudumu, Sadya Awadhi na Wilson Tarimo wenye maua. (Picha na Veronica Mheta).