MAONESHO YA KILIMO

Rais wa Zanzibar, Dk Ali Mohamed Shein (katikati)akipewa maelezo na Mratibu wa Taasisi ya Youth Center Stone Town, Nuru Mtama (kushoto) kuhusu kilimo cha kisasa cha mboga kwa kutumia mbolea inayotokana na taka za majumbani wakati alipofungua Maonesho ya Kilimo yaliyokwenda sambamba na Maadhimisho ya Siku ya Chakula Duniani, Unguja jana. Kushoto kwake ni Makamu wa Pili wa Rais, Balozi Seif Ali Iddi na Waziri wa Kilimo, Maliasili, Mifugo na Uvuvi, Hamad Rashid Mohamed (kulia kwake). (Picha na Ikulu).