MAFUNZO YA AFYA YA KUJAMIIANA NA UZAZI

Washiriki wa mafunzo ya Afya ya kujamiiana na uzazi wakichekecha uelewa wao katika kujipima kwa mafunzo yaliyotolewa katika Shule ya Sekondari ya Chwaka Tumbe, Micheweni kisiwani Pemba. Mafunzo hayo yaliendeshwa na Shirika la Kimataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) na kufunguliwa na Mkuu wa Wilaya ya Micheweni, Salma Khatib Mbarouk. ( Na Mpigapicha wetu).