Waziri amgeuzia kibao Kitwanga

KATIKA hali isiyokuwa ya kawaida, Waziri wa Maji na Umwagiliaji, Gerson Lwenge amemjia juu Mbunge wa Jimbo la Misungwi, Charles Kitwanga akimtaka kama hayuko tayari kukitetea chama chake tawala, Chama Cha Mapinduzi (CCM), ni vyema akajiondoa au kukihama kabisa chama hicho.

Kauli hiyo ya Lwenge kwa Kitwanga aliyewahi kuwa Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi kabla ya kutenguliwa Mei 20, mwaka jana, ilikuja wakati akijibu hoja mbalimbali zilizoelekezwa wizarani kwake na alionesha kukerwa na kauli za mbunge wa Misungwi aliyedai Serikali haijafanya lolote katika jimbo lake.

Kitwanga wakati anachangia bajeti ya wizara hiyo, alisema kama Serikali haitampa miradi ya maji atakwenda kuhamasisha wananchi kwenda kuzima mtambo wa umeme ulioko katika eneo la Ihelela ambako unazalisha maji, jimboni Misungwi.

Akihitimisha bajeti ya wizara yake ambayo ilipitishwa juzi usiku na bunge, Lwenge alisema kama Kitwanga hakitetei chama chake ambacho ni mwanachama na amechaguliwa kuwa mbunge kupitia chama hicho, basi akihame.

“Kama anaona serikali haijafanya chochote wakati imepeleka miradi mingi katika jimbo la lake, basi ajitoe kwenye chama,” alisema Lwenge. Lwenge alisema badala ya kuhamasisha wananchi kutunza miundombinu, mbunge huyo anadiriki kusema atahamasisha wananchi kuharibu miundombinu hiyo.

Alisema Kitwanga ambaye alichangia hoja hiyo kwa mhemuko mkubwa kwamba wizara hilo haijafanya lolote katika jimbo lake, si mkweli kwa sababu kuna miradi mingi inatekelezwa katika jimbo lake na mkoa wa Mwanza kwa uj