TRA yaongeza muda wa kulipa kodi ya majengo

Baada ya kuwepo kwa msongamano mkubwa katika vituo mbalimbali vya Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) wa wananchi wanaolipa kodi ya majengo, mamlaka hiyo imeongeza muda wa kulipia kodi za majengo hadi Julai 31, mwaka huu.

Mkurugenzi wa Idara ya Huduma na Elimu kwa Mlipakodi, Richard Kayombo ametoa taarifa ya kuongeza muda wa kukusanya kodi za majengo kwa mwaka 2016/2017 leo wakati akizungunza na vyombo vya habari.

Amesema wataendelea kukusanya kodi hizo hadi Julai 31 bila adhabu na baada ya hapo watakaochelewa kulipa watalipa pamoja na adhabu.