Mafuta ya nchi jirani yaingizwa Tarime, Rorya

BIASHARA ya magendo ya petroli, dizeli na mafuta ya taa kutokana nchi jirani ya Kenya, imeonekana kushamiri katika wilaya za Tarime na Rorya mkoani Mara, ikiwa ni siku chache baada ya Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) kuamua kuvifungia vituo vya mafuta ambavyo havijafunga mashine za kielektroniki za kutoa risiti (EFDs).

Hayo yamefichuliwa na baadhi ya wafanyabiashara na vijana wanaonufaika na biashara hiyo. Wamedai kuwa kufungwa kwa vituo vya mafuta, kumeleta neema kwao, kwani huingiza kwa magendo ya mafuta wakitumia usafiri wa magari madogo, pikipiki na hata baiskeli kutoka Kenya katika mji wa Isebania, unaopakana na mpaka wa Sirari.

Mji wa Sirari wenyewe una vituo sita vya mafuta, ambavyo viko umbali wa kuanzia meta 20 kutoka mpaka wa Tanzania na Kenya. Hali hali hiyo inayoonekana kuhujumu mapato ya Serikali kwa kuingiza bidhaa za magendo ambazo hazilipiwi kodi.

Baadhi ya wafanyabiashara hao, wakiwemo Michael Marwa, Peter Zakaria na Mwangwa Mathayo, walielezea kuguswa na kufungiwa vituo vyao, kiasi cha kutaka waongezewe muda wa kufunga mashine mpya kwa kuwa shughuli nyingi zimekwama