'Chagueni viongozi kwa kutanguliza maslahi ya Taifa sio binafsi'

WAZIRI wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Dk Harrison Mwakyembe amewataka viongozi wapya wa Shirikisho la soka Tanzania TFF, kutanguliza maslahi ya mchezo huo mbele na sio maslahi yao binafsi.

Mwakyembe aliyekuwa Mgeni Rasmi kwenye Uchaguzi huo wa TFF, unaoendelea kwenye ukumbi wa St. Gasper mkoani Dodoma, alisema Wajumbe ambao ndiyo wapiga kura ndiyo wenye jukumu kubwa la kuhakikisha soka la Tanzania linaendelea.

“Viongozi bora huibuliwa na wajumbe makini wanaoongozwa na dhamira njema na uzalendo usiotetereka kwa vishawishi, alisema na kutaka mgombea atakayeibuka kuwa mshindi kula kiapo kuwa atafanya kazi yake wa uadilifu na kwa manufaa ya watanzania