Dk Mwakyembe: Tengenezeni kanzidata ya wasomi wa Kiswahili

Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dk Harrison Mwakyembe amelitaka Baraza la Kiswahili Tanzania (BAKITA) kuhakikisha inatengeza kanzidata ya vijana wasomi wa lugha ya kiswahili wenye uwezo wa kufundisha lugha hiyo duniani kote.

Dk Mwakyembe ameyasem hayo leo wakati alipotembelea katika ofisi za Baraza hilo zilizopo Kijitonyama, Mnispaa ya Kinondoni jijini Dar es Salaam ambapo amesema ni lazima kuwepo na kanzidata hiyo itakayoorodhesha watalaamu wenye uwezo wa kufundisho lugha hiyo ikiwa watatakiwa katika nchi yoyote dunian.

"Tunatakiwa tujiandae, nchi yoyote ikitaka mwalimu wa Kiswahili tunapeleka, najumbuka tulishindwa kupeleka kwa Rais mmoja alitaka mwalimu, hii ni aibu na ni kutojiandaa," amesema Waziri Mwakyembe.

Mtendaji Mkuu wa BAKITA, Selemani Sewangi amesema, baraza hilo lina changamoto nyingivikiwamo uhaba wa fedha hali inayosababisha baraza hilo kushindwa kufanya shughuli zake kwa ufanisi.