‘Chini ya miaka tisa wasipande pikipiki’

JESHI la Polisi nchini limewakumbusha waendesha pikipiki nchini kutopakia watoto wenye umri chini ya miaka tisa katika vyombo hivyo kwa kuwa ni moja ya suala walilokatazwa katika sheria za usalama barabarani.

Kamishna Msaidizi wa Polisi ambaye ni Ofisa Mnadhimu wa Kikosi cha Usalama Barabarani Tanzania, Theopista Mallya alisema hayo Dar es Salaam jana wakati akizindua kipindi cha BodaBoda kitakachokuwa kikirushwa kupitia televisheni.

Kamishna Msaidizi Mallya alisema jeshi hilo limeshafanya mazungumzo ya mara kwa mara na madereva hao wa pikipiki maarufu kama bodaboda, wakiwa na madarasa mbalimbali ili wapate elimu yenye kuwasaidia katika utoaji wa huduma zao.

Alisema madereva hao ni muhimu wazingatie sheria za usalama barabarani ikiwa ni pamoja na makatazo ya kuendesha bila kofia ngumu, kuwa na abiria zaidi ya mmoja na kumuendesha mtoto wa miaka chini ya tisa