Rais Magufuli amteua Ibrahim Hamis Juma kuwa Jaji Mkuu

RAIS wa Tanzania Dk John Pombe Magufuli amemteua Profesa Ibrahim Hamis Juma kuwa Jaji Mkuu wa Tanzania.

Kwa mujibu wa taarifa kutoka Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais Ikulu, uteuzi huo unaanza leo Septemba 10, 2017. Kabla ya Uteuzi huo Profesa Ibrahim Hamis Juma alikuwa Kaimu Jaji Mkuu wa Tanzania ambapo alichukua nafasi hiyo kutoka kwa Jaji Mkuu Mstaafu Mohamed Chande Othman ambaye amestaafu.

Taarifa hiyo ya Ikulu inasema Profesa Ibrahim Hamis Juma ataapishwa kesho Septemba 10, 2017 saa nne asubuhi Ikulu Jijini Dar es Salaam.