Vigogo wa DART waachiwa huru

Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu imewaachia huru vigogo watatu wa Mradi wa Mabasi yaendayo Haraka (DART) baada ya kuthibitisha upande wa mashitaka kushindwa kuthibitisha mashitaka dhidi yao.

Huku hiyo imetolewa leo na Hakimu Mkazi Mkuu, Respicios Mwijage ambapo amesema, baada ya kupitia ushahidi uliotolewa na mashahidi 10 wa upande wa mashitaka, vielelezo na uashahidi wa utetezi ameona upande wa mshitaka kushindwa kuthibitisha mashtaka yote yaliyokuwa yakiwakabili.

Walioachiwa huru ni aliyekuwa Mtendaji Mkuu wa Mradi huo, Asteria Mlambo, Mkurugenzi wa Fedha na Utawala, Evodius Katale, Mwanasheria Mkuu wa DART, Francis Kugesha na Mkurugenzi wa kampuni ya Yukan, Yuda Mwakatobe. Mashitaka yaliyokuwa yakiwakabili vigogo hao ni uhujumu kwa kula njama na kusababisha serikali hasara ya Sh milioni 83.5.