Wizara yapiga marufuku wanafunzi kuolewa

WIZARA ya Elimu na Mafunzo ya Amali, imepiga marufuku mwanafunzi wa shule kuolewa wakati akiwa katika elimu ya msingi.

Hayo yalisemwa na Naibu Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali, Mmanga Mjengo Mjawiri wakati akijibu swali la mwakilishi wa jimbo la Chakechake, Suleiman Sarhani Said aliyetaka kujua sheria ya ndoa ni mtoto wa umri gani anayestahili kuolewa na kwa upande wa dini ya Kiislamu unasemaje.

Akifafanua zaidi alisema kwa mujibu wa sheria ya Elimu namba 6 ya mwaka 1982, ni marufuku kwa mtoto wa kike kuolewa wakati akiwa katika elimu ya msingi. Alisema elimu ya msingi na maandalizi hutolewa bure na serikali ambapo wazazi wanatakiwa kuhakikisha kwamba wanatoa haki ya watoto wao kupata elimu hiyo.

Aidha alisema kwa upande wa dini ya Kiislamu kwa mujibu wa sheria mtoto akibalehe kuanzia umri wa miaka 9 hadi 12 anaweza kuolewa