Serikali kuendelea kuimarisha sheria za kazi ili kulinda wafanyakazi wa majumbani

SERIKALI imesema itaendelea kuimarisha utekelezaji wa sheria za kazi ili kulinda haki za wafanyakazi wa majumbani pamoja na kujenga uelewa wa wadau kuhusu matakwa ya mkataba na haki za kisheria.

Kauli ya Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Ajira na Vijana, Anthony Mavunde ameyasema hayo wakati akijibu swali la Mbunge wa Viti Maalum, Ritta Kabati aliyeuliza kikwazo kinachokwamisha kuridhia mkataba wa Shirika la Kazi Duniani(ILO)namba 189 na kazi za staha kwa wafanyakazi wa majumbani wakati LESCO imeshapendekeza kuridhia.

Amesema Tanzania kama nchi mwanachama wa ILO ilishiriki kikamlifu katika majadiliano na upitishwaji wa mkataba wa kimataifa wa LO wa wafanyakazi wa majumbani namba 189 wa mwaka 2011 ambao unalenga kukuza kazi za staha kwa wafanyakazi wa majumbani .

“Serikali inathamini mchango wa wafanyakazi wa majumbani katika kujenga uchumi wan chi. Hii ndiyo maana Bunge lako tukufu lilitunga sheria ya Ajira na Mahusiano kazini namba sita ya mwaka 2004 ambayo inazitambua haki za wafanyakazi wa majumbani kama livyo kwa wafanyakazi wengine,” amesema.