Kigwangalla amlipua Nyalandu bungeni

Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk. Hamis Kigwangalla amemtuhumu aliyepata kuwa waziri wa wizara hiyo, Lazaro Nyalandu kutumia madaraka yake vbaya katika kipindi cha miaka miwili alichodumu katika Wizara hiyo.

Dk Kigwangalla ameyasema hayo wakati akichangia Mpango wa Maendeleowa Taifa wa mwaka 2017/2018 ambapo amesema, Nyalandu aliisababishia serikali hasara ya Sh billion 32 kwa kushndwa kusaini sheria ya tozo kwa hoteli za kitali.

Aidha, Dk. Kigwangalla amemtuhumu Nyalandu kuwa na mahusiano na mwekezaj wa kigeni mwenye makampuni ya kitalii nchini na kutumia Helikopta inayomilikiwa na mwekezaj huyo katika kipind cha kutafuta ridhaa ya kuteuliwa kuwa mgombea urais, huku kampuni hizo zikituhumiwa kwa ujangili.

“…Kama kilio chako ni kuchukuliwa hatua, mimi nitaagiza hapa TAKUKURU na Polisi wayasikilize haya nayosema, wachukue hansad wakafanye uchunguzi ili waweze kumchukulia hatua ndugu Nyalandu, wala hilo halisumbui kama hiyo ndo kiu yako wewe kama mwananchi na Mbunge kwamba kwanini Nyalandu hajafika mahakamani, mahakama bado zipo na jinai haiishi muda hata miaka mia ipo tu,” amesema Dk Kigwangalla.