Wafanyabiashara Mikoa yote wapewa siku 14 EFD

KAMPUNI ya Advatech Offi ce Supplied Ltd, wakala wa Serikali anayeuza na kuhimiza matumizi ya mashine za EFDs imetoa siku 14 kwa wafanyabiashara kupeleka uthibitisho wa malipo ya EFD kati ya mwaka 2013/2017.

Meneja wa Fedha wa kampuni hiyo, Saada Miraji alisema jana lengo la kuwataka wafike ofisini ni kupata muda wa kuoanisha matumizi ya kifaa hicho na malipo yaliyofanyika. “Naomba wafanyabiashara mfanye hima mlete risiti mapema bila hivyo mtajiharibia, “alisema.

Aidha katika mkutano huo, Saada alisema wafanyabiashara wengi wamekuwa wazito kutumia mashine za EFD kwa sababu wanazozijua wao wenyewe lakini zaidi ni tabia ya ubahili ya kutotaka kununua mashine hizo.

Alisema wanataka wafanyabiashara na watoa huduma wote wanunue mashine hizo kutunza kumbukumbu zao za mauzo na kulipa kodi. Alisema ni vyema wananchi wote wanaohusika na biashara wafahamu makundi yao kulipa kodi kuwa na mashine ili kwenda sambamba na awamu ya tano katika ufanisi na ulipaji kodi.