Madaktari wa china: wagonjwa njooni tuko kamili

MKUU wa Safari ya Meli maalumu kutoka China, Meja Jenerali Guan Bailin, amewahakikishia Watanzania kuwa meli hiyo inavyo vifaa vyote na wataalamu wa kutosha kutoa huduma hivyo, wananchi wasiwe na hofu na badala yake, wajitokeze kwa wingi kupata huduma zinatolewa bila malipo.

Alisema hayo jana, baada ya meli hiyo kuwasili meli hiyo na kupokewa na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda, katika Bandari ya Dar es Salaam. Makonda alitoa mwito kwa wananchi wenye magonjwa ya kawaida kutoa nafasi kwa wagonjwa wenye magonjwa yaliyoshindakana ili wahudumiwe wapate dawa na huduma hizo.

Meli hiyo yenye madaktari bigwa na wataalamu wa afya zaidi ya 380 itatoa huduma za magonjwa mabalimbali yakiwemo figo, saratani, ini, moyo, macho, sukari, presha pamoja na operesheni mbalimbali Wananchi wakiwa kwenye foleni kusubiri kusajiliwa kwa ajili ya italiwa nchini kwa siku tano.

Alisema ujio wa meli hiyo ni fursa kwa wananchi wa mkoa huo hasa wale wenye magonjwa yaliyoshindikana ambao wamekosa matibabu kwa kutokuwa na uwezo hivyo ni vyema wenye magonjwa ya kawaida wakatoa fursa kwa watu hao ili waweze kupatiwa huduma.

“Tunaowaomba wananchi asije mtu wa mafua hapa tutoe nafasi kwa watu wenye matatizo makubwa wapate huduma,” alisema Makonda. Alisema meli hiyo ambayo itatoa huduma kwa wagonjwa 600 kwa siku imewadia ikiwa salama pamoja na watoa huduma na vifaa vyote vimekamilika hivyo kilichobaki ni wananchi kufika kwaajili ya kupatiwa matibabu.

“Meli hii yenye vifaa vya kisasa itakuwa na vyumba vinane kwa ajili ya operesheni pamoja na vyumba viwili vya wagonjwa mahututi ambavyo vina vitanda 20 hivyo operesheni zote kubwa zitafanyika hapa,” alisema.

Aidha alisema timu ya wataalamu zaidi ya 30 wamekwenda katika baadhi ya hospitali za Mkoa huo ikwemo Amana, Mwananyamala, Temeke, Ocean road kwaajili ya kuangalia vifaa vilivyoharibika kwaajili ya kufanyiwa ukarabati ikiwa ni ombi la mkuu wa Mkoa. Makonda amewataka wananchi watakaokwenda kwaajili ya kupata huduma wafike Makao Makuu ya trafiki kwaajili ya kupewa utaratibu wa kuingia kwenye meli hiyo.