Jaffo ataka uwajibikaji kwa watumishi TAMISEMI

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Suleiman Jaffo amewataka watenda wa serikali za mitaa kuanza kuwajibika kwa kiwango kikubwa na thamani yao ya kazi ionekane katika gurumu la uwajibikaji.

Amewataka watumishi wote walioko chini ya Wizara yake kuwajibika ipasavyo na kwamba wawe na uwezo wa kufanya kazi sehemu yoyote watayopelekwa waweze kufanya kazi vizur.

Jaffo ameyasema hay oleo wakati akifungua, semina ya siku tatu ya Uwazi na Uwajibikaji kwa vongozi waandamizi wa Mamlaka za Serikali za Mitaa. “Kuna watu wengine ukiwahamisha ofisi, anaogopa hata kufanya kazi anajiona hatoshi, akiingia katika ofisi nyingine majukumu yake ukimpa anajiona hawezi kuyafanya, mtu yuko tayari kukimbia hata kazi… kuna akifika ofisini wiki nzima anaongopea tumbo linamuuma kumbe anaangalia namna gani anatafanya kazi, kwa sababu hajajiandaa kisaikolojia,” amesema Waziri Jaffo.