'Ugeugeu' wamuua Ali Abdullah Saleh nchini Yemen

Aliyekuwa rais wa Yemen Ali Abdullah Saleh ameuawa katika mapigano na washirika wake wa zamani wa Kihouthi katika mji mkuu wan chi hiyo Sanaa.

Tukio hilo linafuatia hatua ya Rais huyo hapo juzi kuamua kuiunga mkono Saudi Arabia katika mashambulizi yake dhidi ya waasi hao wa kishia wanaoungwa mkono na Iran.

Baada ya rais huyo wa zamani kutangaza kwamba sasa yuko tayari kufungua ukurasa mpya akiwa na maana kuwa anataka kufanya mazungumzo na utawala wa Saudi Arabia, mgogoro mkubwa kati ya wafuasi wa Saleh na waasi hao kupambana usiku kucha kuamkia leo.

Hatua hiyo ya Saleh ndiyo imesababisha mgawanyiko huo na kuongeza chuki kati yake na waasi wa Houthi. Mgogoro huo umesababisha hofu ya kuzuka mapinago mapya katika nchi hiyo inayokabiliwa na machafuko.

Watu wapatao 8,750 wameuwawa tangu majeshi yanayoongozwa na Saudi Arabia yalipoanza operesheni yake nchini Yemen dhidi ya waasi hao wa kishia wanaoungwa mkono na Iran.