Katibu wa Mbunge wa CCM atiwa mbaroni kwa kugawa rushwa

TAASISI ya kuzuia na kuapambana na Rushwa (Takukuru) Mkoani Mbeya inamshikilia Katibu wa Mbunge jimbo la Rungwe, Amon Sauli kwa tuhuma za kugawa fedha kwa baadhi ya wajumbe wa Mkutano Mkuu wa Uchaguzi wa CCM Mkoa.

Katibu huyo aliyetajwa kwa jina la Ezekiel Mwalusamba, anadaiwa kukamatwa na maafisa wa Takukuru, juzi katika viwanja vya ukumbi wa Tughimbe uliopo jijini Mbey ambako mkutano huo wa uchaguzi ulikuwa unafanyika.

Naibu Kamanda wa Takukuru Mkoa wa Mbeya, Julieth Matichi alithibisha kuwa ni kweli kuna mu wanamshikilia kwa tuhuma za kugawa fedha kwa baadhi ya wajumbe wakati wakati uchaguzi wa Viongozi wa CCM ukiendelea.

Akithibitisha taarifa hizo, Naibu Kamanda wa Takukuru mkoani Mbeya, Julieth Matichi, alisema ni kweli kuna mtu wanayemshikilia kwa tuhuma za kutoa hela kwa wajumbe, wakati wa uchaguzi mkuu huo wa mkoa.