Mkuu wa Mkoa aagiza polisi, hospitali, manispaa kukatiwa maji

MAMLAKA ya MajiaSafi na Usafi wa Mazingira Manispaa ya Sumbawanga mkoani Rukwa (Suwasa) inazidai taasisi za serikali na watu binafsi zaidi ya Sh milioni 310 ikiwa ni malimbikizo ya madeni ya maji huku yenyewe nayo ikidaiwa zaidi ya Sh 100.6 kutoka kwa wadeni wake.

Wadeni hao sugu wanaodaiwa na Suwasa ni pamoja na Jeshi la Polisi, Hospitali ya Rufaa ya mkoa wa Rukwa, Chuo cha Walimu Katandala na Manispaa ya Sumbawanga ambapo kwa jumla zaidi ya Sh milioni 69 huku watu binafsi wakidaiwa zaidi ya Sh milioni 250.

Kufuatia hali hiyo Mkuu wa mkoawa Rukwa Joachim Wangabo amewagiza Suwasa iwakatie maji wadaiwa wote sugu huku akiwataka walipe madeni yao na utaratibu wakulipamadeni uheshimiwe.

Alitoa maagizo hayo alipofanya ziara yake ya kwanza kutembelea miradi inayosimamiwa na Suwasa pamoja na kuufahamu kwa kina mradi wa Maji safi na usafi wa mazingira katika miji saba nchini Sumbawanga ikiwemo, chini ya MDG – Initiative unaofadhiliwa na Serikali na Umoja wa Ulaya (EU) pamoja na Serikali ya Ujerumani kwa pamoja ikiwa nathamania yazaidi ya Sh bilioni 31.

Aidha ameisisitiza mamlaka hiyo kwa kushirikiana na Manispaa pamoja na vyombo vya usalama kuhakikisha vyanzo vya maji vinahifadhiwa na kupiga marufuku wale wote wanaofanya shughuli za kibinaadamu katika vyanzo vya maji na kuwachukulia hatua wale wanaokiuka sheria hiyo ya mazingira.

Kwa upande wake Mkurugenzi Mtaendaji wa Suwasa Mhandisi Hamis Makala alimweleza Wanaboakuwa hadi Novemba mwaka 2017, Suwasa ilikuwa ikidaiwa zaidia ya Sh milioni 100.6 kutoka kwa wadaeni wake.

Alisema, mgawanyo wa madeni ni pamoja na dawa ya kutibu majia Sh milioni 14.5, Mamlaka ya Mapato nchini (TRA), Sh milioni 13, Mamlaka ya Udhibiti wa Nishati na Maji (Ewura) Sh milioni 6.8.

Aliongeza kuwa madeni mengine ni pamoja na fidia ya zaidi ya Sh milioni 32, Shirika la Umeme nchini (Tanesco) Sh milioni 17, mita za maji Sh milioni 6.0 na Manispaa ya Sumbawanga Sh milioni 11 ikiwa ni malipo ya hati miliki.

Katika hatua nyingine, Suwasa imedai kuwa uwezo wake wa kujiendesha umeshuka kwa kiwango kikubwa kutokana na kuongezeka kwa gharama ya undeshaji. Mhandisi Makala alisema kuwa gharama za uendeshaji zimeongezeka kutoka wastani wa matumizi ya Sh milioni 150 kwa mwezi kutoka wastani wa Sh milioni 85 kwa mwezi kuanzia Mei , 2016.