Mume, mke kortini kwa heroin

WAFANYABIASHARA watatu wakiwemo wanandoa, wamefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu wakikabiliwa na kesi ya uhujumu uchumi wa kusafirishaji dawa za kulevya aina ya heroin zenye uzito wa gramu 375.20.

Washtakiwa hao ni Minda Mfamai, Fatuma Mpondi na Oswini Mango ambao ni mke na mume walifikishwa mahakamani hapo jana mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Wilbard Mashauri.

Wakili wa serikali, Adolf Mkini alidai washtakiwa wanakabiliwa na kosa la usafirishaji wa dawa za kulevya aina heroin zenye uzito wa gramu 375.20. Alidai washitakiwa walitenda kosa hilo Novemba 22, mwaka huu maeneo ya Chamazi kwa Mkongo jijini Dar es Salaam.