Bunge halijamtelekeza Tundu Lissu - Ndugai

SPIKA wa Bunge, Job Ndugai amesema Bunge halijamtelekeza Mbunge wa Singida Mashariki, Tundu Lissu (Chadema) aliyelazwa nchini Kenya.

Alisema hayo akizungumza na waandishi wa habari jana kuhusu nafasi zilizo wazi katika majimbo ya Kinondoni na Siha. Akijibu swali juu ya madai ya Bunge kutomjali Mbunge Lissu (Chadema) aliyelazwa nchini Kenya, Ndugai alisema suala la Lissu bado liko mikononi mwa Polisi na si kweli kwamba wamemtelekeza.

Alisema baadhi ya wabunge wamekuwa wakienda kumjulia hali na hata Tume ya Huduma za Bunge ilituma wajumbe wake wawili ambao ni wabunge pamoja na Ofisa Mwandamizi wa Bunge.

“Tume ya Utumishi wa Bunge ndiyo tume mwajiri tulipeleka uwakilishi,” alisema Ndugai na kuongeza kuwa Bunge liko karibu sana na jambo hilo, japo mambo mengi yamekuwa yakisemwa kuhusu Bunge kutomtendea haki, huwezi kubishana na mgonjwa aliye kitandani, kwanza haipendezi.

“Mambo ya kiserikali na kibunge yanakwenda kwa makaratasi hayaendi kwa kuzungumza na waandishi wa habari, jambo hili halikubaliki kumekuwa na lawama nyingi kwenye vyombo vya habari,” alieleza.

Alisema suala la Lissu limekuwa likichanganya watu, kwani mambo mengi yamekuwa yakisemwa, lakini ukweli ni kuwa wabunge wote wamekuwa wakitibiwa kwa usawa. Alisema pia kumekuwa na hoja ya kwa nini Spika hakwenda kumuona Lissu.

“Lissu alipata ajali hiyo Septemba 7, mwaka huu wakati huo ulikuwa ni uchaguzi wa Kenya. Agosti 8, mwaka huu uchaguzi Kenya ulifanyika na kulikuwa na sintofahamu katika masuala mbalimbali,” alifafanua.

Katika siku za karibuni katika mahojiano mbalimbali na vyombo vya habari mbunge huyo amekuwa akidai kutelekezwa na Bunge. Hata hivyo pamoja na wabunge hao kumtembelea Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan alikwenda kumjulia hali na kumfikishia salamu za Rais John MaguTundu Lissu fuli