Mwaka 2017 una mengi ya kukumbukwa: Wema Sepetu mara njano mara bluubluu

Miss Tanzania huyu wa mwaka 2006 aliyepewa jina la ‘Tanzania Sweetheart’ aliuteka uwanja wa siasa baada ya Februari mwaka huu kuikacha CCM na kutangaza kujiunga na Chadema ikiwa ni siku chache tangu ajumuishwe kwenye tuhuma za kutumia dawa za kulevya.

Hapa katikati kukawa na mwendelezo wa ‘series’ nyingi za muvi ya kukihama chama hicho kabla ya mapema mwezi huu kuamua kuimaliza kwa kutangaza tena kurejea CCM akidai sasa ameamua kurejea nyumbani ili awe na amani maana huko alikokuwa hakuwa na amani yoyote.

Mengi bado yanazungumzwa kuhusiana na uamuzi wake huo ingawa bado mwenyewe hajafafanua kwa kina kilichotokea mpaka akachukua uamuzi huo.