Mwaka 2017 una mengi ya kukumbukwa: Lulu anaingia, Babu Seya anatoka

Hii ndiyo imeendelea kuwa habari ya mjini mpaka sasa.

Ikiwa ni siku chache zimepita tangu tasnia ya Bongo Muvi kuingiwa na majonzi baada ya Elizabeth Michael ‘Lulu’ kuhukumiwa kwenda jela miaka miwili kwa kuua bila kukusidia, ghafla inaibuka faraja baada ya kutolewa jela familia ya Babu Seya.

Nguza Viking ‘Babu Seya’ na mwanawe, Johnson Nguza ‘Papii Kocha’ walihukumiwa kifungo cha maisha tangu mwaka 2004 kabla ya Desemba 9, mwaka huu Rais John Magufuli kutangaza kuwasamehe wanamuziki hao na kubadili upepo wa majonzi ya Lulu kuwa furaha kwa wapenzi wa burudani kutokana na tukio hilo.