Mambo manne yanayotishia usalama EAC yatajwa

WAZIRI wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Augustine Mahiga amesema kuna aina nne za mambo yanayotishia usalama katika nchi za Afrika Mashariki.

Mambo hayo ni ya ugaidi, uharamia, majanga kama matetemeko ya nchi, pamoja na ya kisiasa. Balozi Mahiga alisema hayo juzi wakati akifunga mafunzo ya ‘Ushirikiano Imara 2017’, jijini Dar es Salaam, ambayo nchi za Afrika Mashariki zimeshiriki ambazo ni Tanzania, Kenya, Uganda, Rwanda na Burundi.

Alisema licha ya tishio hizo, bado majeshi ya usalama yapo imara, na Tanzania mpaka sasa haijafikia hatua ambayo inatishia amani. Alisema kwa mara ya kwanza mazoezi hayo yamefanyika Tanzania, yanadumisha uzalendo na kubadilishana mawazo.

“Zoezi hili ni la muhimu sana na sehemu ya itifaki. Mwaka jana yalifanyika nchini Kenya. Leo ni fursa ya uongozi wa juu kabisa katika majeshi ya Afrika Mashariki kukaa pamoja na kufanya mazoezi pamoja na Tanzania tumekuwa wenyeji,” alisema Balozi Mahiga.

Kwa upande wake, Mnadhimu Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi, Luteni Jenerali James Mwakibolwa alisema malengo ya mafunzo hayo ni kubadilishana uzoefu na namna gani kitu fulani kikitokea kifanyike vipi. Luteni Jenerali Mwakibolwa alisema mafunzo hayo pia yanaongeza ufanisi na weledi katika majeshi, yalifunguliwa Desemba 4, m