Mnadhimu JWTZ aapishwa, bosi mpya JKT ateuliwa

Amiri Jeshi Mkuu amemwapisha Mnadhimu Mkuu wa Jeshi la Ulinzi wa Wananchi ya Tanzania (JWTZ), Luteni Jenerali Yakubu Mohamed katika hafla iliyofanyika Ikulu, Dar es Salaam leo.

Tukio hilo pia liliambatana na Mkuu wa JWTZ, Jenerali Venance Mabeyo kuwavisha vyeo vya meja jenerali 10 ambao kabla ya uteuzi wao, waliokuwa na cheo cha brigedia. Aidha , mkuu huyo ametangaza mabadiliko kadhaa katika jeshi hilo ikiwemo kumteua kumteua Meja Jenerali Martin Busungu kuwa Mkuu wa Jeshi la Kujenga Taifa (JKT).

Akizungumza mara baada ya kula kiapo hicho, Mnadhimu Mkuu Luteni Jenerali Yakubu Mohamed amemshukuru Rais Nagufuli kwa kumwamini na hatimaye kumteua katika wadhifa wake wa sasa huku akiahidi kulitumikia jeshi hilo kwa weledi na kulinda misingi na taratibu zilizopo.