Munishi atemwa Taifa Stars

KIPA wa Yanga, Deogratius Munishi ‘Dida’ ameachwa katika kikosi cha wachezaji 23 wa timu ya Taifa, Taifa Stars, kitakachoingia kambini Jumanne kujiandaa na mchezo wa kirafiki dhidi ya Lesotho utakaochezwa Juni 10, Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.

Akizungumza na wandishi wa habari jana, Kocha Mkuu wa Taifa Stars, Salum Mayanga alisema wachezaji wataingia kambini na mazoezi yataanza Mei 24-29 Dar es Salaam na Mei 30 watakwenda kuweka kambi Misri kwa wiki moja.

Kikosi kamili cha Taifa Stars ni makipa Aishi Manula (Azam), Benno Kakolanya (Yanga) na Said Mohammed (Mtibwa). Mabeki; Shomari Kapombe, Erasto Nyoni na Aggrey Morris (Azam), Hassan Kessy, Mwinyi Mngwali (Yanga), Mohammed Hussein ‘Tshabalala’na Abdi Banda (Simba), na , Salim Abdallah (Mtibwa).

Viungo: Himid Mao na Salum Abubakar ‘Sure Boy’(Azam), Said Ndemla, Muzamil Yassin, Jonas Mkude na Shiza Kichuya (Simba), Simon Msuva (Yanga), Farid Mussa (DC Tenerife).

Washambuliaji: Thomas Ulimwengu (FC Eskilstuna, Denmark), Mbwana Samatta (KRC Genk, Ubelgiji), Mbaraka Yussuf (Kagera Sugar), Ibrahim Ajib (Simba) na Abdulrahman Mussa (Ruvu Shooting). Benchi la ufundi ni Kocha Mkuu Salum Mayanga akisaidiwa na Fulgence Novatus, kocha wa makipa, Patrick Mwangata, Meneja ni Dani Msangi, Madaktari Gilberti Kigadiya na Richard Yomba na mtunza vifaa Ally Ruvu