Kocha awapa somo wachezaji

TIMU ya Vijana waliochini ya miaka 17, ‘Serengeti Boys’ huenda ingepata ushindi wa mabao mengi kama ingetumia vizuri nafasi zilizotengenezwa wakati wa mchezo dhidi ya Angola wa kundi B ya michuano ya Afcon 2017.

Akizungumza kwa njia ya simu Kocha msaidizi wa Serengeti Boys, Oscar Mirambo alisema, wachezaji wanapaswa kufahamu umuhimu wa nafasi zinazopatikana na kuzitumia. “Kwa sasa kwa maana ya kufanya mazoezi hakuna kitu ambacho unaweza kufanya kutokana na muda ulivyo, kitu ambacho unaweza kukifanya kuwajenga kisaikolojia ‘mental training’ ili watoto waweze kuelewa umuhimu wa nafasi wanazozipata na kuwa makini kuzitumia,” alisema Mirambo

“Mechi ya kwanza tulikuwa tunazuia na hatukuwa na namna sahihi ya kushambulia kulingana na mpinzani tuliyekutana nae, mechi dhidi ya Angola tulijaribu kushambulia, tuliruhusu watoto washambulie na tunashukuru tukaweza kufunga mabao mawili,” “Kama tungekuwa na mipango ya kushambulia tangu mechi ya kwanza inawezekana matokeo yangekuwa tofauti tungeweza kutengeneza nafasi nyingi na kupata matokeo,” alisema Mirambo Serengeti Boys ilishinda mabao 2-1 dhidi ya Angola na kufikisha pointi 4 sawa na Mali ambao nao walishinda 2-1 dhidi ya Niger.

Kesho kutwa Serengeti boys itaingia uwanjani kucheza na Niger mchezo wa mwisho katika hatua ya makundi na timu mbili za juu zitafuzu nusu fainali na kukata tuiketi ya kucheza Kombe la Dunia kwa vijana, nchini India, Oktoba