Kilichojiri mkutano wa Rooney na vyombo vya habari

Meneja wa Everton Ronald Koeman amemkabidhi Wayne Rooney jezi yenye namba 10 mgongoni baada ya straika huyo kuihama Manchester United.

Katika mkutano wake wa kwanza na vyombo vya habari baada ya kurudi Everton, Rooney amesema kuwa anafarijika kurejea Everton baada ya kuondoka miaka 13 kuichezea United na kunukuliwa na BBCSport akisema kuwa “sijarudi nyumbani kustaafu.

Ninataka kucheza na kuwa na mafanikio katika klabu hii.” "Nilikuwa na wakati mzuri nikiwa Manchester United lakini soka husonga mbele na wachezaji husonga mbele,” amenukuliwa nahodha huyo wa zamani wa United ambaye leo ameanza mazoezi na Everton leo. Rooney anachukuwa namba ya jezi iliyokuwa ikivaliwa na straika Romelu Lukaku anayetimkia Old Traford.