Timu za Yanga na Simba u20 zawasili jijini Mbeya

Timu za Yanga na Simba u20 zimewasili jijini Mbeya kwa ajili ya kushiriki mechi za hisani maalumu kwa ajili ya kuchangia mfuko wa udhamini wa ukimwi.

Akizungumzia maandalizi hayo msemaji wa Tume ya Taifa ya kudhibiti ukimwi Tanzania TACAIDS, Elizabeth Kaganda, alisema kuwa timu zote tayari zimewasili na zipo katika hali nzuri.

Mechi hizo zinaanza rasmi hii leo kwa timu ya Yanga kukipiga na Mbeya City katika mchezo wa ufunguzi. Mchezo wa pili itakuwa ni kati ya Simba na Tanzania Prisons kesho na mechi zote zikipigwa Uwanja wa Sokoine jijini Mbeya.

Mchezo wa fainali utachezwa jumamosi kwa kuzikutanisha timu washindi wa tar 27 na 28 kuanzia saa tisa na nusu alasiri. Aidha Kaganda alitaja viingilio vya mchezo huo kuwa ni sh 3000 mchanganyiko na 10000 kwa VIP.