Simba yaendelea kuongoza

SULUHU na Azam FC imeshindwa kuiondoa Simba kileleni mwa msimamo wa Ligi Kuu Tanzania Bara katika mchezo uliofanyika Azam Complex Chamazi, Mbagala jijini Dar es Salaam.

Sare hiyo imeifanya Simba kufikisha pointi nne huku ikitamba na mabao yake saba iliyoyapata katika mchezo wa ufunguzi ilipocheza dhidi ya Ruvu Shooting na kushinda 7-0 kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.

Prisons ya Mbeya wenyewe walishindwa kutumia vizuri Uwanja wao wa nyumbani wa Kumbukumbu ya Sokoine baada ya kulazimishwa sare ya mabao 2-2 na Majimaji 2-1 ya Songea na hivyo kufikisha pointi nne.

Wajelajela hao kama wangeshinda jana wangeweza kuongoza ligi hiyo kwani wangefikisha pointi sita kabla ya mechi za leo, ambapo Mbeya City itakuwa nyumbani dhidi ya Ndanda FC ya Mtwara, Mtibwa Sugar itacheza dhidi ya Mwadui FC kwenye Uwanja wa Manungu.

Mechi zingine leo ni Singida United itaikaribisha Mbao FC ya Mwanza kwenye Uwanja wa Jamhuri Mjini Dodoma. Katika mchezo wa jana, Simba ilitawala zaidi kipindi cha kwanza na dakika tatu tangu kuanza kwa mchezo, Nicholas Gyan nusura afunge kama siyo uimara wa kipa wa Azam Fc, Razak Abalora kuokoa.

Dakika ya 18 Azam walilikaribia lango la Simba na kushambulio la nguvu lakini Wnock Agyei nusura afunge lakini alishindwa kutumia vizuri nafasi aliyopata na mpira ukadakwa na kipa Aishi Manula wa Simba.

Mchezaji wa zamani wa Azam, John Bocco licha ya kumpiga chenga kipa wa timu hiyo lakini alishindwa kuukwamisha mpira wavuni baada ya kuteleza. Wakati huohuo, mabingwa watetezi Yanga leo wanashuka dimbani kucheza na Njombe Mji katika moja ya mechi zitakazopigwa leo. Kocha msaidizi wa Yanga Shadrack Nsajigwa amesema kuwa hawataidharau Njombe Mji lakini wana uhakika wa kushinda