Ratiba Ligi Kuu Zanzibar hadharani

CHAMA Cha soka Zanzibar ZFA Taifa kimepanga ratiba ya ligi Kuu ya Zanzibar inayotarajiwa kuanza September 15 mwaka huu.

Ratiba ya ligi hiyo ilipangwa kwa ushirikiano wa pamoja kati ya viongozi wa kamati tendaji na vilabu chini ya mkurugenzi wa Ufundi wa chama hicho Abdulghani Msoma. Kwa mujibu wa ratiba ya ligi hiyo mchezo wa kwanza utakuwa ni kati ya Mafunzo na mabingwa watetezi JKU.

Jumla ya timu 14 zitashiriki ligi hiyo ambayo kwa jana ratiba hiyo lipangwa kwa mzunguuko wa kwanza na wa pili. Msoma amesema kuwa wameamua kupanga ratiba hiyo kwa kushirikisha vilabu ili kuweka uwazi na kuepukana na malalamiko ya timu kuona  imeonewa juu ya upangaji wa ratiba hiyo.

Hata hivyo vilabu hivyo mbali ya kupanga ratiba lakini pia walipatiwa block registration za usajili. Klabu zinazoshiriki ligi hiyo ni Mafunzo, JKU, Kipanga, Miembeni City, Jang'ombe Boys, Taifa ya Jang'ombe, Polisi, KVZ, Chuoni, Black Sailor, Charawe, Zimamoto, KMKM na Kilimani city.