Polisi yapiga marufuku ‘Jogging’ barabarani bila vibali

KIKOSI cha Usalama barabarani Mkoa wa Dar es Salaam kimepiga marufuku vikundi vyovyote vinavyoathiri vikiwemo vile vya mazoezi ya kukimbia, bila kupata kibali.

Mkuu wa Kikosi cha Usalama barabarani mkoa huo, Marison Mwakyoma ametoa maelekezo hayo wakati akizungumza katika mahojiano ya ana kwa ana na HabariLeo, jijini Dar es Salaam leo (Jumanne).

Ameshauri kuwa ili kikundi kiweze kufanya jambo lolote ambalo kwa namna moja ama nyingine litaathiri matumizi ya barabara ni lazima kipate kibali kutoka kwa Mkuu wa Jeshi la Polisi. Marufuku hiyo imetolewa baada ya uwepo wa vikundi maarufu vya ‘Jogging’ ambavyo vimekuwa vikifanya mazoezi katikati ya barabara jambo ambalo linaathiri matumizi ya barabara.

Kwa undani wa taarifa hii, soma HabariLeo kesho Jumatano