Bashiri Aziz Mwanamitindo anayejivunia utofauti wa ngozi yake

BASHIRI Aziz ni mwanamitindo mwenye ugonjwa wa ngozi ujulikanao kama vitiligo (mabaka meupe mno), lakini pamoja na changamoto hiyo, kebehi na kauli za chuki dhidi yake, ameamua kuishi kwa raha zake.

Vitiligo ni ugonjwa unaotokana na kinga ya mwili kushambuliwa na seli zinazoitwa kitaalamu melanocyte ambazo ndizo zinazotengeneza rangi nyeusi tuliyonayo mwilini. Kauli za kebehi ambazo amekuwa akikutana nazo mwanamitindo huyo ni pamoja na wengine kumwambia anafanana na pundamilia, wengine wakimwaminia ana madoa doa kama ng’ombe, na baadhi ya kauli zilimuathiri.

Haikuwa rahisi kuishi na ugonjwa wa vitiligo. Bashir Aziz, mfanyabiashara wa Uingereza aliyegeukia uanamitindo na mwanaharakati anatafakari changamoto ya kuwa wa tofauti na namna alivyojifunza kuishi na hali yake ya mabakabaka.

Vitiligo ni ugonjwa unatokana na kinga ya mwili kushambuliwa seli zinazoitwa kitaalamu melanocyte ambazo ndizo zinazotengeneza rangi nyeusi tuliyonayo mwilini. Kuishi na vitiligo, mwanamitinndo na mwanaharakati huyo siku zote alijihisi ni mtu wa tofauti, lakini pamoja na changamoto hiyo, kebehi na kauli za chuki dhidi yake, aliamua kujikubali na kuishi kwa raha zake.

Muda ulivyozidi kwenda ndivyo Aziz alikubali muonekano wake wa kipekee na hivi karibuni alikuwa kwenye mlolongo wa picha mpya za Mpigapicha Brock Elbank, #Vitiligo. Mpigapicha Brock ameamua kujitoa kuonesha upekee na uzuri wa watu wanaoishi na vitiligo.

Mtazamo wake mtaalamu huyu wa lensi na bingwa wa picha anaamini uzuri uko machoni mwa mtu. “Kuishi na vitiligo imekuwa changamoto. Kama mtoto, nilikuwa najitambua sana nilipokuwa nikifanya vitu vya kawaida, kwa sababu tu watu walikuwa wakinishangaa.

Nilikuwa nikivaa kofia kibao, kwani ulikuwa huwezi kupishana nami mtaani bila kuona nywele zangu. Hata kwenye kuogelea nilivaa fulana. Hali hii iliharibu kabisa kiwango changu cha kujiamini nikiwa mdogo sana,” anasema Aziz.

Anasema jambo gumu ni kukabiliana na mtu asiyefahamu tofauti ya kuungua au alama ya kuzaliwa. “Njia pekee iliyonisaidia kukabiliana na changamoto hii ilikuwa kujifunza kujikubali.

Miaka ilivyhata bora zaidi. Utofauti lazima uadhimishwe; angalia kilichopo nje na utashangaa utakachobaini,” anasema. Aziz anasema kila siku watu wanaangalia vitu vipya, sura mpya, mitindo mipya na kwamba wanavutiwa zaidi na utofauti, wigo mpana wa mawazo na kukubali ukweli kuwa kila mtu ana upekee kwa namna yake.

Ni kawaida watu wengine ni tofauti, wakiwa na nywele tofauti, alama tofauti mwili, mabaka, lakini kila mtu ni wa pekee. “Sio lazima kiwe kitu kinachoonekana kama vitiligo, kipekee kumbatia tu chochote ulichonacho. Uzuri ni kuwa na mchanganyiko wa sifa zinazokufanya wa pekee, ndani na nje,” anasema.

Aziz anasema ukweli kuwa jamii siku hizi ina uelewa zaidi kumemuwezesha kujiamini zaidi, kujipenda zaidi na kuonesha uzuri kwa dunia miongoni mwa vingi. “Hakuna cha kuogopa chochote, dunia inakuwa kubwa na ang’avu zaidi pale unapokubali ujinga ukisukume… acha kebehi, chuki kuwa moto wa utakaotumia kukung’arisha,” anasema.

Kebehi, chuki na unyanyasaji wa watu dhidi ya Bashir Aziz kuwa anaonekana kama ng’ombe, mara kama pundamilia ndivyo vimempaisha leo hii ni mwanamitindo anayejivunia hali yake na dunia imemfahamu.