Makala Maalum: Mambo ya kuzingatia mnyukano wa udiwani

LEO wananchi katika kata 43 zilizoko katika mikoa 19, wanaenda kupiga kura katika uchaguzi mdogo wa madiwani.

Mkurugenzi wa Uchaguzi wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) Kailima Ramadhani anaeleza mambo kadhaa ambayo wapiga kura na wadau wengine wa uchaguzi wanatakiwa kuyazingatia.

Swali: Nani anastahili kwenda kupiga kura katika uchaguzi wa leo?

Wenye haki ya kwenda kupiga kura leo ni wale wote ambao walijiandikisha kwenye daftari la Wapiga Kura lililotumika katika Uchaguzi mkuu wa mwaka 2015. Jumla ya wapiga kura 333,309 ndiyo ambao wanategemewa kupiga kura katika uchaguzi huu wa leo. Vyama vyote vya siasa vilishapewa nakala tepe (soft) ya Daftari hili, hivyo ni vema kila chama kikampatia nakala mango za vituo husika mawakala wao ambao watakuwa kwenye vituo vya kupigia kura. Ila tuwakumbushe tu vyama vya siasa kuwa nakala ya tume katika kituo ndiyo nakala itakayokuwa sahihi iwapo kutatokea tofauti.

Swali: Wale ambao wamepoteza kadi ya kupigia kura itakuwaje?

Jibu: Matumizi ya vitambulisho hivyo yatazingatia masharti yafuatayo: Mpiga kura awe aliandikishwa kwenye Daftari mwaka 2015. Majina yake yawe katika orodha ya wapiga kura katika kituo husika. Majina na herufi za majina hayo yaliyopo katika kitambulisho yafanane kwa herufi na mtiririko na yale yaliyopo katika Daftari.

Sura iliyopo katika kitambulisho ifanane na iliyopo katika daftari. Hati ya Kiapo (Affidavit) cha kuthibitisha majina zaidi ya majina yaliyomo kwenye Daftari hakitaruhusiwa kutumika. “Lengo la Tume ni kuwapa fursa na haki walioandikishwa kuwa wapiga kura, lakini wangeweza kuikosa haki hayo kwa kukosa kadi za upigia kura sababu ya kupotea au kuharibika au kuchakaa.”

Swali: Kuna vituo vingapi vya kupigia kuwa na mambo gani ya kuzingatiwa kwenye vituo?

Jibu: Vituo 884 vitatumika kupiga kura. Vituo hivi ndivyo vilivyotumika mwaka 2015. Wasimamizi wa uchaguzi watavipatia Vyama vya Siasa vinavyoshiriki uchaguzi mdogo vitapatiwa orodha ya vituo vya kupigia Kura. Orodha ya wapiga kura ilishabandikwa katika kila Kituo cha Kupigia Kura tangu tarehe 19 Novemba, 2017 ikiwa ni siku nane kabla ya siku ya upigaji kura na hivyo kila mpiga kura aende kwenye kituo chake ambako jina lake ilibandikwa.

Swali: Kwenye vituo vya kupigia kura kutakuwa na mawakala wa vyama, kazi yao ni ipi?

Jibu: Kazi za Mawakala wa upigaji kura, Kutambua wapiga kura, Kuwakilisha na kulinda maslahi ya mgombea au wagombea katika kituo cha kupigia kura; na Kazi nyingine ni kushirikiana na msimamizi wa Kituo na Wasimamizi. Wasaidizi wa kituo ili kuhakikisha taratibu zinazohusu upigaji kura na uchaguzi zinafuatwa.

Swali: Leo ni siku ya kupiga kura, vituo vitafunguliwa saa ngapi?

Jibu: Vituo vya kupigia Kura vitafunguliwa saa 1.00 asubuhi na vitafungwa saa 10.00 jioni. Baada ya saa 10:00 jioni askari atasimama nyuma ya mtu wa mwisho aliyepo kwenye mstari.

Swali: Baada ya upigaji kura kukamilika, kura zitahesabiwa wapi?

Jibu: Kura zitahesabiwa katika vituo vya kupigia kura [kituo cha kupigia kura kitageuka kuwa cha kuhesabia kura baada ya upigaji kura kukamilika.] Hata hivyo kwa sababu za kiusalama msimamizi wa kituo kwa kushauriana na Mawakala wa upigaji kura anaweza kuelekeza kura zikahesabiwe eneo lililo jirani litakalofaa tofauti na lile ambalo kura zimepigwa.

Swali: Utaratibu gani unatumika kuhesabu kura?

Jibu: Kifungu cha 82 cha sheria ya uchaguzi, jukumu la kutangaza matokeo ni la Tume ya Taifa ya Uchaguzi. Matokeo ya vituo vyote vya kupigia kura katika Kata husika hujazwa kwenye Fomu Na. 24C mbele ya mwakala wa kujumlisha matokeo. Msimamizi Msaidizi wa Uchaguzi baada ya kujiridhisha na kuthibitisha matokeo ya kura za kila Mgombea atatangaza mgombea aliyepata kura nyingi zaidi halali kuwa ndiye mshindi.

Kifungu cha 86 kinafafanua kuwa kutokuwepo kwa mawakala wakati wa upigaji au kuhesabu au kujumlisha kura katika muda na mahali palipoteuliwa hakutabatilisha utekelezaji wa majukumu ya Tume yaliyofanyika kwa mujibu wa Sheria, Kanuni na Taratibu.

Swali: Tunafahamu kuwa uchaguzi huu unahusisha waangalizi wa uchaguzi. Nini wajibu wa waangalizi hao?

Jibu: Watazamaji wa Uchaguzi wa ndani ndiyo wanaoruhusiwa katika uchaguzi mdogo. Kazi ya Watazamaji wa Uchaguzi ni kuona kama uchaguzi unafanyika kwa mujibu wa Katiba, Sheria, Taratibu, Kanuni za uchaguzi na Maelekezo yaliyotolewa na Tume ya Taifa ya Uchaguzi.

Watazamaji watafanya kazi yao baada ya kukubaliwa na kupewa idhini na Tume ya Taifa ya Uchaguzi. Hatakiwi kuingilia kwa namna yoyote kazi na majukumu ya Tume ya Taifa Uchaguzi.

Swali: Waandishi wa Habari ni muhimu katika kuripoti uchaguzi huu, je tume imeandaa mazingira ya waandishi kufanya kazi kwa ufanisi?

Jibu: Kipengele cha 9.15 cha kitabu cha Maelekezo kwa wasimamizi wa uchaguzi kinafafanua kuwa Waandishi wa Habari wanaruhusiwa kuingia katika Vituo vya kupigia kura kwa idhini ya msimamizi wa uchaguzi.

Swali: Una ujumbe gani kwa wapiga kura na vyama vya siasa?

Jibu: Vyama vya Siasa vitatimiza wajibu wao ipasavyo na kuhamasisha wanachama wao walioandikishwa kuwa Wapiga Kura wajitokeze kwa wingi kwenda kupiga kura leo kumchagua diwani wanayemtaka.

Ni imani ya tume kuwa viongozi wa vyama vya Siasa watakuwa chachu ya ku- Nyota/ Mapishi waongoza na kuwaelekeza wanachama, wafuasi na mashabiki wao katika kushiriki uchaguzi kwa amani na utulivu.