TWFA ni mfano mzuri

HIVI karibuni Chama cha Soka cha Wan a w a k e (TWFA) kilifanya uchaguzi mkuu wa viongozi wake, Dar es Salaam.

Katika uchaguzi huo, Mwenyekiti Amina Karuma alitetea kiti chake kwa kupata kura 47 kati ya 52 za wapiga kura wote. Nafasi ya Makamu Mwenyekiti ikichukuliwa na Rose Kissiwa kwa kura 42.

Mwanahabari mwandamizi wa gazeti la Nipashe, Somoe Ng’itu alishinda nafasi ya Katibu Mkuu kwa kuvuna kura 49. T h e r e s i a M u n g ’ o n g ’ o alishinda nafasi ya Katibu Msaidizi na Hilda Masanche akashinda nafasi ya Mweka Hazina.

Alipata uhazini kwa kupata kura 25 wakati mhariri msaidizi wa michezo wa gazeti hili, Zena Chande akishinda ujumbe wa Mkutano Mkuu wa TFF kwa kura 44. Wajumbe Triphonia Temba, Mwamvita Kiyogoma, Jasmine Soudy na Chichi Mwidege hawakushinda uchaguzi.

Walitoswa baada ya wagombea wote wanne kutopata zaidi ya nusu ya kura kulingana na idadi ya wapigakura kwa mujibu wa kanuni za katiba ya TWFA. Kwanza niwapongeze waliofanikiwa kutetea nafasi zao na wale walioingia kwa nafasi tofauti kwa mara ya kwanza.

Kushinda kwenu kumeonesha kuwa mnaaminiwa na mnaweza kufanya mapinduzi ya kimaendeleo kwa kuendeleza soka la wanawake kuzidi kuelekea pazuri. Bila shaka ushindi mkubwa mlioupata hautawafanya kubweteka na kujisahau.

Tunategemea mtatoa ushirikiano mkubwa, umoja na mshikamano katika kuendeleza soka kwa wanawake nchini. Soka la wanawake lina changamoto nyingi na wengi wenu kwa sababu ni wazoefu mnazijua hivyo, wadau na mashabiki wa soka watapenda kuona mnazifanyia kazi.

Lakini pia wajumbe ambao hawakushinda kwa sababu ya kura zao hazikutosha, imeonesha wazi kuwa demokrasia inakua. Kushindwa kupita hata mmoja ina o n e s h a dhahiri kuna tatizo na ndio maana wapiga kura w a m e o n a waangalie weledi wenu na kutumia demokrasia kuwanyima nafasi ya kuendelea kulitumikia soka la wanawake.

Napongeza hatua hiyo na iwe fundisho kwa wengine ambao wamekuwa ni waoga wa kupambana na wale ambao hawafai. Kutochaguliwa kwa wajumbe hao kunaweza kuwa ni somo kwa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) ambalo linatarajia kufanya Uchaguzi Mkuu wake Agosti 12, Dodoma. Bila shaka kunaweza kuwepo kwa viongozi waliopitishwa na wanaotiliwa shaka kuwa wameingia kwa maslahi binafsi na sio kuendeleza soka la Tanzania.Waachwe